Katika hali isiyokuwa a kistarabu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba Mh Sammuel Sitta amelazimika kuhairisha bunge baada ya kutokea kutoelewana kwa wajumbe na wabunge wa bunge la katiba.
Chanzo cha mtafaruku huo ni baada ya Wajumbe na Baadhi ya wabunge wa upinzani kupinga Jaji warioba asiwasilishe rasimu ya katiba leo mpaka Rais ahutubie Bunge hilo kwanza.Mwenyekiti wa Bunge akaruhusu Jaji Warioba aendeleee na Uwasilishaji lakini wabunge wakaanza kujibizana na kupiga makofi na meza za bunge.Baadhi ya wajumbe wametoka nje na wengine wamebaki ndani huku wakiwa wamesimama.