Urusi yashutumiwa kwa kujaribu kuligawanya bara Ulaya

Majeshi ya Urusi yameiteka kambi ya kijeshi katika eneo la Crimea kwa kutumia magari yasiyopenya risasi na maguruneti hapo jana.Hatua hii inakuja siku moja baada ya Rais wa Urusi Vladimir Putin kutia saini sheria inayolitambua rasmi jimbo la Crimea kama sehemu ya himaya ya shirikisho la Urusi.Majeshi ya Ukraine yanaripotiwa pia kuikimbia kambi ya jeshi la majini baada ya kushambuliwa na waandamanaji wanaoiunga mkono Urusi na kusalimisha meli mbili za kijeshi kwa majeshi ya Urusi.Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier alikutana jana na waziri mkuu wa Ukraine Arseny Yatseniuk mjini Kiev na baadaye kukutana na viongozi wa biashara mashariki mwa nchi hiyo.Steinmeier amesema Ujerumani inaunga mkono umoja wa Ukraine na itapinga jaribio lolote la kuigawanya nchi hiyo na kuishutumu Urusi kwa kujaribu kuligawanya bara la Ulaya.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company