Wawakilishi wa vyama vya upinzani wakiwemo kundi dogo la kikomunist na vyama vya congress walijitokeza barabarani huko mji wa kaskazini Khartoum
AFP,Na RFI
Jeshi la polisi nchini Sudan limetumia gesi ya kutoa machozi kuwatanya waandamanaji wa vyama vya upinzani jana usiku mwandishi wa habari wa AFP ameripoti licha ya serikali ya nchi hiyo kutoa wito wa mazungumzo ya kitaifa.
Takribani wawakilishi mia mbili wa vyama vya upinzani wakiwemo kundi dogo la kikomunist na vyama vya congress walijitokeza barabarani huko mji wa kaskazini Khartoum wakiimba kwa sauti ya juu ''Uhuru na haki''.
Polisi walitumia risasi za mpira na gesi ya kutoa machozi dhidi ya kundi la waandamanaji ambao walitawanyika huku wakiwarushia askari mawe.
Wanachama wa upinzani waliandamana baada ya mkutano katika makao makuu ya chama cha Sudan Congress kujadili hali ya mambo nchini humo ikiwemo uasi, umaskini na mgogoro wa kisiasa.