Wanaharakati wa Uganda wataka sheria ya mepnzi ya jinsia moja kusitishwa

Muungano wa mashirika ya raia ya kutetea haki za binadamu wamekwenda mahakamani kuomba mahakama ya kikatiba ifutilie mbali sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja ambayo wanasema inakiuka katiba pamoja na haki za binadamu.
raia wa Kampala walisoma jarida la "Red Pepper" Feb. 25, 2014.
Vita kati ya serikali ya Uganda na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu sasa vimepelekwa mahakamani. Muungano wa mashirika ya raia ya kutetea haki za binadamu wamekwenda mahakamani kuomba mahakama ya kikatiba ifutilie mbali sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja ambayo wanasema inakiuka katiba pamoja na haki za binadamu.Mwandishi wa Sauti ya Amerika mjini Kampala Leylah Ndinda anaripoti kwamba, mawakili wanaowawakilisha mahakamani wapenzi wa jinsia moja wanaiomba mahakama isitishe kwa mda utekelezaji wa sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja hadi pale mahakama itakapotoa uamuzi.
Pia waliiomba mahakama iamrishe vyombo vya habari viache kujapisha picha, majina na anwani za wapenzi wa jinsia moja. Baada ya rais Yoweri Museveni kutia saini mswada dhidi ya mashoga tarehe 24 mwezi uliopita, magazeti mawili yamekuwa yakichapisha picha za watu wanaodhaniwa kuwa mashoga.

" Unampiga mtu picha na unachapisha kwenye gazeti lako kwamba huyo mtu ni shoga. Unafanya nini? Unamuweka hadharani auliwe. Sio haki kabisa."

Profesa Ogenga Latigo mwanasiasa na mwanasayansi anasema sheria hii inakandamiza haki za binadamu na Uganda haikuwa na haja ya kuweka sheria ya kupinga ushoga lakini wangeweka sheria ya kuzuia ushoga ili watu wasiwahamasishe wenzao kuiga ushoga. Aliongezea kusema watu wanafaa kujua kwamba

Walalamikaji kwenye kesi hii wanasema kuna maswala ambayo wangetaka mahakama ichunguze kwa sababu kwa maoni yao sheria hii mpya haiambatani na katiba.

Nicholas Opiyo, raia wa Kampala anasema, "bunge liliupitisha mswada huu likiwa halina idadi ya kutosha ya wabunge na hilo likakiuka kipengele cha themanini na nane na tisini na nne cha katiba yetu, mswada huu ambao unakiuka usawa kwa wote kama inavyosisitizwa na katiba. Adhabu ya kifungo cha maisha kwa watu watakaopatikana na hatia ni kali sana na haiambatani na kosa ambalo watakuwa wamelitenda na unakiuka haki ya binadamu kutopewa adhabu za kikatili ambazo zinashusha hadhi yao."

Baadhi ya mashoga nchini Uganda wanalalamika kuwa baada ya rais Museveni kutia saini sheria dhidi ya mashoga, maisha yao yamekuwa hatarini.

David Bahati mbunge aliyeuwasilisha mswada dhidi ya mashoga bungeni akizungumzia hatua ya wanaharakati hawa kwenda mahamani alisema, "Tunawatakia kila la kheri."

Mahakama ya kikatiba baada ya kupokea ombi lao haikusema ni lini kesi hii itaanza kusikilizwa.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company