ASIA IDAROUS AWIKA NA MAVAZI YA UBUNIFU NCHINI NIGERIA, AUPAISHA MUUNGANO WA TZ

Na Andrew Chale 

MBUNIFU mkongwe wa mitindo nchini, Asia Idarous Khamsin mwishoni mwa wiki aliweza kuitangaza vyema Tanzania katika onyesho kubwa la mavazi ya ubunifu lililokuwa maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lililofanyika Abuja, Nigeria.
Onyesho hilo la aina yake, lililofanyika kwenye hoteli ya Kimataifa ya Nyota tano ya Sheraton Abuja, usiku wa April 25, huku likiudhuriwa na watu wengi wakiwemo watanzania na raia wengine wa kigeni walioongozwa na balozi anayewaiwakilisha Tanzania, nchini humo Balozi Daniel Ole
Njoolay.
Akizungumza na mtandao huu, kwa njia ya simu kutoka Abuja, Nigeria, Asia Idarous ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions, aliwashukuru watanzania kwa kuandaa onyesho hilo maalum, kwani limeweza kuitangaza Tanzania kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo ya ubunifu, biashara na utalii.
"Hii ni heshima kwangu na kwa Tanzania, kwani wenzetu Wanaigeria wamevutika na bidhaa zetu nyingi zikiwemo zile tulizotumia kwenye mavazi ya ubunifu. Hivyo nasema hii ilikuwa ni nafasi ya kipekee kuwavuta kuja nchini kwa fursa za kiuchumi na uwekezaji” alisema Asia Idarous.
Alisema baadhi ya bidhaa ikiwemo khanga, vikoi, batiki na mashuka ya wamasai kutoka Tanzania, yalitia fola na kuvutia wengi wakiwemo raia wa Nigeria na wageni wengine waliofika kwenye sherehe hizo.
Sherehe hizo mbali na kuhudhuriwa na balozi wa Tanzania, pia mabalozi mbalimbali wa mataifa wengine nao walijumuika kwa pamoja kwenye onyesho hilo. Wengine ni pamoja na Mkurugenzi wa Montage Ltd, Teddy Mapunda, Fatma Mwinyi, Salma Maulid na wengine wengi.
“Utanzania wetu ni Muungano wetu, tuulinde, tuumalishe na kuudumisha ndani na nje ya mipaka yetu, hakika onyesho hili pia litaendelea kuwa la kuongeza tija ya umoja wetu ikiwemo watanzania waishio nje ya mipaka yao ‘Diaspora’” alisema Asia Idarous.
Nigeria ni miongoni mwa nchi pekee zenye kudumisha utamaduni wake ukiwemo wa mavazi yenye kuwatambulisha watu wa jamii hiyo, tasnia ya ubunifu na mitindo imekuwa ikipewa kipaumbele hali inayopelekea tija na hata Taifa hilo kuwa juu kiuchumi.

Mwisho
Caption:
Displaying 1-Asia Idarous akiwa na vazi la Kitanzania.JPG
Asia Idarous akiwa na vazi maalum alilolibuni ambalo lilitia fola kwenye onyesho hilo @ Sheraton Hotel Abuja Nigeria


Displaying 2- keki ya miaka 50 ya muungano wa Tanzania , Abuja Nigeria.JPG
Keki ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania, iliyoandaliwa na watanzania, Abuja Nigeria. 
Displaying 3-Fatma Mwinyi.JPG
Fatma Mwinyi akiwa kwenye pozi katika onyesho hilo la miaka 50 ya muungano Abuja NigeriaDisplaying 4-Tanzanian family @#AbujaNigeria.JPG



famil,y wakiwa kwenye picha ya pamoja nyumbani kwa balozi, Balozi Ole Njoolay, Abuja Nigeria Displaying 5-SheratonAbuja.JPG Sheraton Hotel Abuja Nigeria presenting Fashion Tanzania @ Muungano Tanzania Inavyoonekana.
Displaying 5-Sheraton Hotel Abuja Nigeria presenting Fashion Tanzania. ikionekana kwa ndani eneo la pool.JPGSheraton Hotel Abuja Nigeria presenting Fashion Tanzania. ikionekana kwa ndani eneo la pool
Displaying 6-Asia Idarous & Teddy Mapunda @Sheraton hotel Abuja Nigeria Celebrating MuunganoTanzania.JPGAsia Idarous & Teddy Mapunda @Sheraton hotel Abuja Nigeria Celebrating MuunganoTanzania
Displaying 7-Asia Idarous & Salma  wakiwa kwenye pozi.JPGAsia Idarous & Salma wakiwa kwenye pozi
Mwishoni
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company