AZAM NDIE BINGWA LIGI KUU TANZANIA BARA 2014


Timu ya Azam FC imefanikiwa kutangaza Ubingwa wa Ligi kuu ya Soka Tanzania bara msimu wa 2013/2014 baada ya kuinyika Mbeya City 2-1 mjini Mbeya hii leo.

Azam FC kwa ushindi huo imefikisha pointi 59 ambazo hazitaweza kufikiwa na timu yeyote ile katika ligi hiyo. Azam pia mbali na kuwa bingwa pia imefikia rekodi ya Simba ya mwaka juzi ya kutwaa ubingwa bila kupoteza mchezo hata mmoja.
Azam pia imevunja rekodi ya mwaka 2001 baada ya Ubingwa kwenda Mtibwa Suger badala ya wakongwe Simba na Yanga.

Rekodi hiyo pia inashikiliwa na timu za Coast Union ya Tanga na Tukuyu, Cosmo na Mseto Morogoro.

Yanga imeshinda mechi yake ya leo dhidi ya JKT Oljoro kwa bao 2-1 na kufikisha pointi 55, Mbeya Siti wapo nafasi ya tatu wakiwa wamebaki na pointi 46 wakifuatiwa na Simba ambayo leo nayo imepata kichapo cvha bao 1-0 kutoka kwa Watoto wa mjini Ahanti Unt na kunusurika kushuka daraja.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company