Ban Ki-moon ataoa tahadhari CAR


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema nchi ya Jamuhuri ya Kati haipaswi kuruhusiwa kugeuka kuwa Rwanda nyingine.

Akiandika maoni yake kwenye mtandao wa BBC, Bwana Ban amesema kwamba zaidi ya nusu ya raia wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati wanahitaji msaada wa kibinadamu.

Akihusisha mambo yalivyo Jamuhuri ya Afrika ya Kati na kumbukumbu ya miaka 20 ya mauaji ya halaiki nchini Rwanda, amesema jamii ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua sasa badala ya baadae kuja kuomba msamaha itakapotimia miaka ishirini ijayo.

Siku ya Alhamis Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliwapa mamlaka wanajeshi 12,000 wa Umoja wa Mataifa waliopo nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company