MSHAMBULIAJI Romelu Lukaku ameshuhudia klabu yake, Chelsea ikitolewa katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu, huku kikosi cha Jose Mourinho kikikosa huduma ya mchezaji huyo iliyemtoa kwa mkopo Everton.
Lukaku alikaa mbele na Diego Maradona - aliyehudhuria mechi hiyo pamoja na binti yake Dalma - huku The Blues wakichapwa mabao 3-1 na Atletico Madrid na kupoteza nafasi ya kutinga Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Makocha wa Manchester United, Phil Neville na Paul Scholes pia walikuwepo jukwaani Chelsea ikifutwa kwenye michuano licha ya kutangulia kupata bao kupitia kwa Fernando Torres aliyeifunga klabu yake ya zamani.
Wangeweza wangekuwa nawe: Romelu Lukaku (kushoto) akiangalia Chelsea ikitaabika mbele ya Atletico Madrid
Phil Neville (kushoto) na Paul Scholes walikuwepo pia
Huku Mashetani Wekundu wakiwa tayari wamepoteza matumaini ya ubingwa na kufuzu kwenye Ligi ya Mabingwa msimu ujao, haikufahamika kama wawili hao walikuwa hapo kusaka vpaji kwa niaba ya kocha mkuu wa muda, Ryan Giggs.
Kocha wa England, Roy Hodgson pia alikuwepo na kuna uwezekano alikwenda kumshuhudia Ashley Cole mwenye umri wa miaka 33 kama atamfaa kwenye kikosi chake cha kombe la dunia.
Kocha wa England. Roy Hodgson (katikati) alikuwepo pia
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago