John Kerry aanza ziara yake katika bara la Afrika

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani John Kerry anaanz ziara yake katika baadhi ya mataifa ya bara la Afrika.
REUTERS/Jacquelyn Martin/Pool
Na RFI

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry ameianza ziara rasmi katika mataifa ya Afrika huku akitarajiwa kutembelea mataifa kadhaa yenye kushudia mapigano hususa Sudani Kusini.



Kerry anatazamiwa kutembelea nchi ya Ethiopia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, pia Angola ambapo msemaji wa wizara ya mambo ya nje Jen Psaki anasema ni ziara inayolenga kuyahamasisha mataifa hayo kuhusu masuala ya amani na usalama hali kadhaklika haki za binadamu lakini pia namna ya kuimarisha demokrasia.

Ziara hiyo ya siku 6 itampelekea waziri Kerry kukutana na mashirika ya kiraia, makundi ya vijana, pamoja na asasi za kiraia

Kerry, ambaye anatazamiwa kuhetimisha ziara yake na kurejea mjini Washington may 15, atajadili na wanaharakati wa mashirika ya kiraia ,viongozi ambao ni vijana barani Afrika kuhusu hatma ya bara la Afrika, kuendeleza biashara, kuwekeza pamoja na ushirikiano katika masuala ya maendeleo barani Afrika.

Atakapo wasili katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, Kerry atakutana kwa mazungumzo na viongozi wa Umoja wa Afrika wakiwemo viongozi wa mataifa ya Ethiopia, Kenya na Uganda.

John Kerry anaifanya ziara hio mjini Addis Ababa, wakati huu ambapo kunafanyika mazungumzo kati ya wajumbe wa serikali ya Sudani Kusini na ule wa waasi wanaomuunga mkono makamu wa zamani wa rais aliefutwa kazi, Riek Machar. Mazungumzo hayo yalianza mwanzoni mwa juma hili, baada ya kusimama kwa miezi kadhaa.


Mazungumzo kati ya wajumbe wa serikali ya Sudani Kusini na waasi katika mji mkuu wa Ethiopia,Addis Abeba.AFP / Jenny Vaughan
Mapigano kati ya Jeshi la Sudani Kusini na waasi yamesababisha maelfu ya raia kuuawa na maefu wengine kulazimika kuomba hifadhi katika maeneo yaliyotengwa kwa Umoja wa Mataifa, ambayo yanalindwa na kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini Sudani Kusini.

Makubaliano ya usitishwaji mapigano kati ya pande hizo mbili yalisainiwa januari 23 mwaka 2014 mjini Addis Ababa, lakini bado mapigano yanaendelea kushuhudiwa.

“Tutazifikishia pande hizo mbili ujumbe mkali na kuwaonyesha kwamba iwapo hawatochukua hatua zinazohitajika za kukomesha mapigano, watachukuliwa hatua na jumuiya ya kimataifa”, amesema Kerry, huku akibaini kwamba Washington imekua ikishughulikia orodha ya watu, ambao wanaweza wakawekewa vikwazo.

Hata hivo, waziri huyo wa mashauri ya kigeni wa Marekani hatojielekeza nchini Rwanda, ambayo ni mshirika wa karibu na Marekani, baada ya uhusiano wake na Marekani kulegalega kwa kipindi cha miaka miwili sasa kutokana tuhuma kwamba serikali ya Kigali imekua ikiwaunga mkono waasi wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, M23.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company