KADINALI PENGO,SIASA WAACHIE WANASIASA. Au vua joho na uvae vyuzi za kijani na njano au bluu,kwa Dk.Slaa jifunze.

NA Oscar Samba
Najua sio wakwanza kukwazika na mwenendo wa kiongozi huyu wakidini katika swala hili la kikatiba hapa nchini ila naweza kuwa miongoni mwa watanzania wachache waliodiriki kulikemea hili hadharani.

Ni haki kwa kila mtu kutoa maoni yake na wamazo yake; jamii na vyombo vya dola vyote vyapaswa kuliheshimu hili,hii sio kauli yangu bali ni kauli ya kisheria kutoka kwa mkataba na azimio la Umoja wa Mataifa ambapo Tanzania ni mwanachama na pia ilitilia sahihi kuridhia jambo hili na kubwa zaidi kwa katiba ya Tanzania ya 1976 inalitambua hili katika ibara ya 18 na 19 pia nguvu ya uhuru huu amabo leo ninauchambua inapatika katika ibara 20.

Kuwa na haki ya kunena au kutoa maoni yako hayaingili mipaka ya busara wala hekima,ulishawahi kutafakari ni kwanini wanajeshi na baadhi ya viongozi wa serikali hawaruhusiwi kujiunga na vyama vya siasa.Lakini ni haki yao,je! Ni busara kuhubiri siasa makanisani kama alivyo fanaya Lukuvi hivi majuzi?

Jibu sahihi ni hapana,na jua siku nyingi zilizopita Askofu Kakobe alijitokeza kwenye mkutano wa vyama vya upinzani pae jangwani nakutamka “KATIBA NI MALI YA WANANCHI”kauli hii haikuzua migongano kwani haikuonekana kuwagawa watanzania wala kuwabagua kwani ilikuwa na lengo la kujali masilahi ya watu wote watanzania bila kujali hisia wala sera zao.

Kabla sija kita jembe langu chini na kuanza kuchimbua kilichozikwa chini amabacho ndicho kilicho nifanya ni twae kalamu na dafutari leo embu tafakari nami: Unajua ni kwanini hotuba ya Jaji Warioba haikulaaniwa na wanaharakati badala yake iliibuwa maswali yenye majibu.

Ila hutuba ya Raisi Kikwete ililaaniwa na kupingwa vikali na wanaharakati na wachambuzi wa maswala ya kisiasa hapa nchini huku ikiibuwa maswali yaliyo jaa majibu yenye mashaka na wasiwasi mkubwa?

Kama hujagundua basi jibu lake ni jepesi mno ni kwamba Kadinali Pengo na Raisi Kikwete wamesahau wao ni wakina nani na baya zaidi hawajajiwa lakusema katika mazingira husika?

Sina utamaduni wa kuambatana kimawazo au kimtazamamo na watu ambao hushindwa kuelewa dhamana walizo nazo kijamii wala aingii akilini mtu kutamka ya kwamba alikuwa akitoa maoni yake,bungeni wakati muda wa maoni ulishapita na aliingia akiwa na mabodi gadi na bendera ya kijani ikisalia kwenye gari lake iliyomanisha uwepo wake na cheo chake.

Haiwezekani watanzania wapoteze muda wao kutazama hotuba ya Raisi kisha mtu asiyetafakari kwa kina anakuja na majibu mepesi kama makapi na kusema eti alikuwa akitoa maoni yake,,kweli !! ; huu sio wakati wa te! Te!.

Najua unajiuliza mbona kina Oscar leo anatuanzia na swala la kitambo kidogo la Raisi Angali kichwa cha habari kinamlenga Kadinali Pengo?Tafadhali vuta subira kwani maneno machache ya jayo yana jawabu lake.

Sasa Napata picha pale ninapoanza kufananisha matukio kwa hutuba ya Raisi pale bungeni hususani aliposema ya kwamba kuna asikofu alimfwata na kumshauri ya kwamba serikali tatu haifai.

“Hata siku moja nikiwa ikulu alinifwata kiongozi mmoja wadini na kuniambia ya kwamba sasa matatizo haya yameshindika kwa serikali mbili sasa mnaona mkiongeza ya 3 ndipo suluhu ilipo”Kwa maneno yake anadai eti ya kwamba ni kuongeza matatizo, “hata ushauri huu wa baba asikofu sii mufwate”.

Nina uwakika ya kwamba kauli ya Asikofu tena mwenye cheo cha Kadinali akiwa ndie Askofu mkuu wa kanisa katoliki hapa nchini Pengo haiku sahihi,najua amekuwa akijaribu kujitetea ya kwamba kusema kwake anaunga mkono mfumo wa serikali 2 ni maoni yake na anayo haki ya kufanya hivyo kama nilivyo elezea pale awali katika aya ya pili ya makala hii.

Hainingi akilini eti kwa Asikofu kuingilia maswala ya kisiasa na kuvaa bendera za chama cha siasa bila kujali ya kwamba nyuma yake lipo kundi kubwa ambalo kiuwalisia limevaa na kunywa maji ya bendera mbalimbali nae kulilazimisha kuvaa mavazi ya njano na kijani ni kukengeuka.Mbya zaidi mtazmo huu hutolewa kanisani na mhusika husema ni maoni yake,kweli ! ?

Sina haya wala mshipa wa aibu na kwangu uwoga ni dhambi kubwa mno, siogopi wala kupepesa macho kwa kusema kuwa PENGO kwa hili umepotoka,Ingawaje katiba inakulinda na azimio la umoja wa mataifa ila hukutumia busara kutamka adharani ya kwamba unaunga mkono sera ya CCM ya serikali mbili.Ina wezekana ni kweli kujisaidai haja kubwa ni kwa kuku tuu! na punde afanyavyo hivyo bata huambia ni haja ndogo ila zipo sababu za msingi.

Wala usibwetekea na kufagiliwa na watu wa CCM kwani hao ni wanasiasa na hakika kwao wanakuona kama ngazi ya kupandia kwani wanajua wakifanikiwa ni rahisi kwa wao kutimiza haja zao za kisiasa kwa kuzingatia ya kwamba unaongoza mamilioni ya watu.

Ila Kadinali Pengo umesahau ya kwamba ya Ngoswe mwachie Ngoswe, yaani ya WANASIASA WACHIE WANASIASA.Embu tafakari name ingali kuwaje Mufti mkuu wa waisilamu Shekhe Idi Simba akasimama adharani na kutamka ya kwamba yeye anaunag mkono mfumo wa serikali tatu kama Jjaji Warioba alivyopendkeza.

N ae Askofu Kakobe akasema ya kwamba nae anaunga mkono Muundo wa mkataba,Kwa mitazamo hiyo je! Watanzania hatuaacha kuitazama katima kisisa na kuanza kuitazama kidini?

Je! Mashekhe na Maasikofu hawata anzakujibizana kweye misikiti na makanisa kwa kupanga hoja mbalimbali,? Na kwa bahati nyingine upande moja ukapita na mafumo moja wapo kupitishwa kisha kukatokea kutokuelwana baina ya upande ulioshinda na mwingine kushindwa je! hapo machafuko yatakosa budi kutokea?

Mwaka 2011 tarehe 5 mwezi 2 kulitokea machafuko hapa mkoani Arusha katika maandamano ya kumpinga meya amabae chama cha CHADEMA kilidai ni batili,Je waisilamu wakidai nao ya kwamba kura zimechakachuliwa katika kura za uchaguzi wa kuipitisha rasimu na kuanza kuandamana na kisha kutokea kama ya Arusha ambayo yalihusisha vyama vya siasa na hapa kuwa ni baina ya waksto wakatoliki dhidi ya waisilamu na wakristo wa pentekoste.

Acheni majibu dhaifu ambayo hata mototo wa chekechea awezi kupewa, wakati wakutoa maoni ulisha pita,nanikutaadharishe ya kwamba Kadinali Pengo kumbuka uyafanyayo yanaendelea kuibua maswali yanyokosa majibu dhidi ya tuhuma za waisalmu hapa nchi ya kwamba serikali hii inaongozwa na kanisa Katoliki toka enzi za Nyerere,mie binafsi siliamini hili ila kuona ni kuamini!!!..

Pia ujiandae pale UKAWA watakapoanza kukujibu kwani asili ya wanasiasa ni kujibizana kwa hoja na wakati mwingine vijembe utawala, sidhani kama madili ya kanisa lako yatakuruhusu kujibizana nao na kisiasa usipojibu mapigo mana yake umeshindwa na kushindwa kisisa kwa mwanasiasa ni kufedheheka.

Ushauri wangu kwako, kwamba ikiwezekana futa kauli na ufahamu ya kwamba asikari polisi hata akiwa msalani hapaswi kusahau kuwa yeye ni asikari,pili kama sio tatu siasa wachie wanasiasa na nne na mwisho kama siasa ni tamu kuliko Kanisa usisite kufanya kama DK. Slaa, yaani achia ubadiri na vyaa nyuzi za kisisa na utaamua mwenyewe kama ni njano na kijani au Njano,nyekundu, nyeupe au utaongeza bluu.

Kumbuka injii hufanya wainjilisti na sisa wachie mwanasiasa pia kwa DK. SLAA JIFUNZE.



HATUTAKI YATOKEE TANZANIA KAMA YANYOTOKEAYO HUKO NIGERIA NA AFRIKA YA KATI.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company