KOCHA wa zamani wa Barcelona, Tito Vilanova imeelezwa yupo katika hali mbaya kiafya kwenye kliniki aliyolazwa kwa matibabu.
Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 45 alipepelekwa katika chumba cha dharula jana kwa ajili ya upasuaji baada ya hali yake kubadilika wiki iliyopita.
Vilanova amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya saratani tangu Novemba mwaka 2011 na Redio Nacional imesema anakabiliwa na wakati mgumu.
Mgonjwa: Kocha wa zamani wa Barcelona, Tito Vilanova amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya saratani kwa miaka kadhaa
Amekuwa akitembelewa na ndugu, jamaa na marafiki katika kliniki ya Chiron Clinic alikolazwa.
Kocha huyo alilazimika kujiuzulu mwaka 2013 baada ya kuanza kuzidiwa na maradhi hayo.
Timu yake ilishinda taji hilo, lakini Jordi Roura aliifundisha Barcelona kwa miezi miwili wakati Vilanova aliposafiri kwenda New York kwa matibabu ya saratani, kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Tata Martino msimu huu.
Vilanova (kushoto) awali alikuwa msaidizi wa Pep Guardiola Barca
Vilanova aliteuliwa kuwa kocha wa Barcelona mwishoni mwa msimu wa 2011-12 na akawawezesha Blaugrana kusawazisha rekodi ya Real Madrid kumaliza msimu na pointi 100. Alianza kuwa Msaidizi wa Pep Guardiola mwaka 2008.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago