KOREA KUSINI:JAMAA WA WAHANGA WAAJALI WAPAMBANA NA POLISI


Jamaa wa baadhi ya waathiriwa 250 wa ajali ya Ferry nchini Korea Kusini ambao bado hawajapatikana, wamekabiliana na polisi.

Jamaa hao wanalalamikia kile wanachosema ni kujikokota kwa waokozi wanaowatafuta waathiriwa hao.


Usiku kucha , wapiga mbili walipata miili 17 zaidi baada ya kufanikiwa kuingia ndani ya Ferry hiyo iliyozama kwa mara ya kwanza.
Walinzi wa bahari katika pwani ya nchi hiyo, walishindwa kueleza ni sehemu gani hasa ambapo miili hiyo ilipatikana ndani ya ferry hiyo baada ya kushindwa kuona vyema wakiwa chini ya bahari.
Meli hiyo ilizama siku ya Jumatatu ikiwa imewabeba watu zaidi ya mienne wengi wakiwa wanafunzi wa shuke.
Mawimbi makali na hali mbaya ya hewa inaathiiri shughuli ya kuwatafuta waathiriwa.
Waendesha mashitaka wanasema kuwa wakati wa ajali hiyo kulikuwa na nahodha mwengine asiye na uzoefu aliyekuwa ameshikilia usukani wa meli hiyo.
Nahodha huyo alikamatwa pamoja na nahodha wa ferry hiyo na wafanyikazi wengine.Chanzo BBC Swahili
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company