
Karibu
tena katika mfululizo wa somo hili linalolenga kukujuza kuhusu kujiliwa na Mungu
katika maisha yetu na leo tupo katika sehemu ya pili na ya mwisho ya makala hii
langu jina ni Oscar Samba tafadhali ungana nasi sasa ;yaani mimi na ROHO
MTAKATIFU; Amina.
Lakini
kabla ya kuendele naguswa kukujuza hili,”kumbuka Mungu anapoweka mteule wake
yani kiongozi analokusudi kwako; kwa hiyo hakikisha ya kwamba unafanya kazi
sanjari na mtu huyu pili kumbuka ya kwamba uongozi wa MUNGU hutoka kwa MUNGU
kwa ajili ya kazi yake,fanya hivyo ukifahamu ya kuwa;
MUNGU
NDIYE ANAETEUWA NA KUCHAGUA PILI MUNGU
NDIE ANAEWEKA MAONO YAKE NDANI YAKE (MBEBA MAONO) hakikisha unatembea na maono
ambayo MUNGU ameweka ndani yake.
Sasa tuendele na somo letu:
YAKUPASAYO
ILIUTEMBELEWE/ILI USIKOSE MAJIRA YA KUTEMBELEWA NA BWANA.
Kumbuka
MUNGU hutembelea ili awe na ushirika na sisi kwa hiyo jiandae kupata nguvu za
kipekee za MUNGU.Matendo ya Mitume 3
soma zaidi hapo.
Ukisoma
kitabu cha Ufunuuo utaona jinsi ambvyo Yohana anakutana na Yesu akiwa katika
hali ya tofauti,Kumbuka Yohana alikuwa na ukaribu sana na Yesu hata wakati
wakukaribia kifo chake pale mezani Yohana alikuwa ameketi kifuani mwake.Ufunuo
1:7 na kuendelea utaona wakati ambao MUNGU alimpa ufunuo wa Yesu mfufuka,nae
alipomwangalia alianguka chini kama mfu,anasema ilikuwa ni sauti kama ya maji
mengi kama baragumu,nyele zake zilikuwa nyeupe maneno yake ni kama upanga.
Huo
ndio uliokuwa utukufu ulinong’a kama theluji katika vazi na uso kama jua huku
miguu yake ikiwa kama shaba liiyosuguliwa.Matendo 2:1 tunaona kushuka kwa ROHO
MTAKATIFU aliyeshuka na kufungua mlango wa kuingia katika patakatifu patakatifu
ambapo unadhiirisha ya kwamba wakati wakutembelewa na MUNGU au kujiliwa kwetu
ni wakati wowote.
Wapo
watu ammbao kama wewe hauta wambia ya kwamba YESU anaokoa wataenda jehenamu
kwani uokovu wao unakutegemea wewe,kama Yule kiwete katika kipindi cha
Pentekoste amabapo wakina Petro walimombea,kumbuka katika hekalu hili Yesu
alikuwa akipita mara kwa mara ila hakumuombea.
Ukisoma
katika matendo ya Mitume 3:17 na kuendelea utaona jinsi ambavyo kunasemwa
nyakati au zama hizi kwa undani zaidi;
1.kuburudishwa.
2.Zama
za kufanywa upya (Urejesho) na urejesho huu ni matokeo ya kutembelewa na
MUNGU,hapa nachukuwa kanuni 3 za msingi zinavyoonesha jinsi ya kuingia
1.Luka
19 KANUNI YA ZAKAYO,tunajifunza kuwa na shahuku na hamu ya mambo ya MUNGU
Zakayo alikuwa na shahuku hiyo je! Wewe unayo hiyo shahuku? Kumbuka heri wenye
kiu na shahuku maana hao watashibishwa .Daudi katika Zaburi ya 46 anasema kama “ayala
waioneavyo shahuku maji ya mto divyo nafsi yangu ilivyo na haja nawe”.
Ndugu
yangu na kuombea Mungu auishe hiyo shahuku ndani yako,Kama shahuku hiyo imepungua
na muomba BWANA aiuwishe upya shahuku hiyo tena na tena.Mungu wetu ni Mungu wa
mambo makubwa kwahiyo na wataka wakristo wote duniani kutokuwa legelege.
Shahuku
yako kwa MUNGU isiridhike na mambo madogo madogo,chonde chonde shahuku yako kwa
Mungu isiwe ni ya kuridhika na kutosheka haraka,kwa hiyo Zakayo anatufundisha
kuwa na shahuku ya kudumu .
Kma
shahuku hiyo kwako inasusua tafadhali nguvu ya msalaba iliyo mfufua Yesu krsto
iambatane nawe sasa.
Jambo
jingine amabalo Zakayo anatufunza siku ya leo ni hatua ya IMANI,Zakayo mara
baada ya kumuona YESU aliamua kupanda juu ya mti na hatimae akamuona YESU.Ili
imani yako ifanye kazi ni lazima uchukuwe hatua, na hatua za IMANI ni
kudhubutu.
Mpendwa
unapaswa kuwa shujaa wa IMANI kama Zakayo ambae alifanya
mambo makubwa ambapo watu wasiojua walimcheka ila yeye moyoni alitambua
kilichopo ndani yake na hatimae akafanikiwa.
Kazi ya imani yetu lazima itawaliwe
na matendo, na matendo huja baada ya kudhubutu na hatimae hupata matunda.Tafadhali
tena na tena nakusihii chukuwa hatua za IMANI.
2.KANUNI YA BATHIMAYO KIPOFU, moja kwa
moja aliamini kuwa KRISTO anaweza pili anatufundisha yatupasa kumuita KRISTO
bila kujali watu wanasemaje,tena bila kuchoka wala mashaka au wasiwasi
wowote.Tumia wakati wako kumuita MUNGu.
3.KANUNI YA UAMSHO,fahamu uamsho
unatangulia urejesho,na baada ya uamsho ndipo urejesho hiyo ndiyo tafsiri
yake.Ili tusiyakose majira haya yatupasa kuyaweka maisaha yetu katika mstari.
MWISHO
Nakuatakia sikuku njema
mpendwa na endelea kuitembelea www.mwakasegeinjili.blogspot.com