Russia imesema kuwa, inaangalia jinsi ya kuchukua hatua zinazofaa iwapo nchi za Magharibi zitaendelea kuisakama kuhusiana na mgogoro wa Ukraine. Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov amesema, iwapo nchi za Magharibi zitaendelea kuchukua hatua dhidi ya Russia, Moscow nayo itatoa majibu. Marekani na washirika wake wa Ulaya hivi karibuni waliiwekea Russia vikwazo wakidai kwamba inaingilia masuala ya Ukraine.
Katika upande mwingine Rais Vladmir Putin wa Russia na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron wameafikiana kwamba mgogoro wa Ukraine unapaswa kutatuliwa kwa njia za amani. Viongozi hao wawili wamejadili suala hilo kupitia mazungumzo ya simu ambapo pia wamesisitiza kuendelea kubadilishana mawazo juu ya masuala mbalimbali.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago