Marekani yalaani mauaji Sudan Kusini


Jeshi lilipoteza mji wa Bentiu ambao sasa uko chini ya waasi
Ikulu ya White House imesema kuwa imeshangazwa na mauaji ya kinyama ya mamia ya raia Sudan Kusini na kutoa wito wa kusitishwa kwa msururu wa vurugu zinazoendelea nchini humo.

Umoja wa mataifa ulisema siku ya Jumatatu kwamba waasi waliwauwa mamia ya raia katika mji wa Bentiu na wengi walikufa katika msikiti mmoja, hosipitali na kanisa ambako walikuwa wamekimbilia kutafuta usalama.

Msemaji wa ikulu ya White House, Jay Carney, amesema kuwa rais, Salva Kiir, na kiongozi wa waasi ni sharti watangaze hadharani kuwa mashambulizi dhidi ya raia hayakubaliki.

Maelfu ya watu wamefariki dunia tangu mapigano ya kikabila yazuke mwezi Disemba mwaka uliopita.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company