MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA BUNGE MAALUM LA KATIBA MJINI DODOMA


Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba,ambaye pia ni Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia(kulia) akijadiliana jambo na Madaraka Nyerere ambaye ni mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo. Kushoto ni mjumbe wa Bunge hilo,Leticia Nyerere.

Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu Hassan (katikati) akizungumza jambo na baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo, wakati wanatoka nje katika kikao cha asubuhi.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema(kushoto) akibadilishana mawazo na wajumbe wa Bunge hilo, Shamsi Vuai Nahodha (katikati) na kulia ni Dk. Tulia Akson mara baada ya kikao cha leo asubuhi.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Ezekiah Oluoch, akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma ambapo aliwasisitiza UKAWA kurudi ndani ya Bunge hilo.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Ezekiah Oluoch, akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma ambapo aliwasisitiza UKAWA kurudi ndani ya Bunge hilo.


aadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na mwanasiasa mkongwe, mzee Kingunge Ngombale Mwiru na mjumbe wa Bunge hilo Juma Njumayo aliyevaa mewani mweusi(kulia) baada ya mwanasaiasa huyo. Picha na Magreth Kinabo
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company