Na Prince Akbar, Dar es Salaam
WAWAKILISHI wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), TP Mazembe na AS Vita wamepangwa kundi moja, A katika Ligi ya Mabingwa Afrika kama ilivyo kwa Esperance na C.S Sfaxien za Tunisia ambazo zipo kundi B pamoja na E.S Setif ya Algeria na Ahly Benghazi ya Libya.
Mabingwa mara tano wa michuano hiyo, Zamalek ya Misri wapo pia Kundi A na wababe hao wa DRC na vigogo wa Sudan, Al Hilal.
Vijana wa kazi; Washambuliaji tegemeo wa TP Mazembe, Watanzania Mbwana Samatta kulia na Thomas Ulimwengu kushoto wamepangwa kundi moja na AS Vita ya DRC pia
Mechi zinatarajiwa kuchezwa kuanzia kati ya Mei 16 na 18 na 23 na 25, Juni 6 na 8, Julai 25 na 27, Agosti 8 na 10 na 22 na 24 huku timu zitakazoshika nafasi mbili za juu kwenye makundi zikisonga Nusu Fainali.
MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA:
Kundi A: TP Mazembe (DRC), Al-Hilal (Sudan), Zamalek (Misri) na AS Vita (DRC)
Kundi B: Esperance (Tunisia), CS Sfaxien (Tunisia),
Entente Setif (Algeria) na Al-Ahly Benghazi (Libya).
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago