Rais wa Marekani akiituhumu Urusi kutoheshimu makubaliano ya Geneva na kuendelea kuchochea vurugu nchini Ukraine.
REUTERS/Junko Kimura-Matsumoto/Pool Na
RFIRais wa Marekani Barack Obama ameituhumu Urusi kwa kutoheshimu makubaliano yaliofikiwa hivi karibuni jijini Geneva Uswisi kwa ajili ya kutafutia suluhu mzozo wa Ukraine. Tuhuma hizi za Obama zinakuja baada ya serikali ya Urusi kusema ipo tayari kuingilia kati mzozo wa mashariki mwa Ukraine iwapo faida zake zitawekwa hatarini.
Hatuwa ambayo inakuja baada ya serikali ya Kiev kutangaza kuanzisha operesheni dhidi ya wanaharakati wanaodai kujitenga kwa eneo hilo la mashariki.
Kauli hii ya Urusi inakuja kuhatarisha zaidi hali iliopo wakati huu jumuiya ya kimataifa ikijaribu kulitafutia suluhu ya kudumu swala hilo.
Sergeï Lavrov, waziri wa mambo ya nje wa Urusi, akiituhumu Marekani na Umoja wa Ulaya kujaribu kufanya mapinduzi mapya nchini Ukraine.REUTERS/Denis Balibouse
Wakati huohuo Urusi kupitia waziri wake wa mambo ya nje Sergei Lavrov, imeituhumu Marekani na Umoja wa Ulaya kujaribu kufanya mapinduzi nchini Ukraine.
“Marekani na Umoja wa Ulaya umekua ukijaribu kufanya mapinduzi mapya ya aina yake nchini Ukraine kinyume na katiba”, amesema Lavrov, kituo cha habari cha serikali chini Urusi kimethibitisha.
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema iwapo faida zao zitashambuliwa kama ilivyokuwa katika eneo la Ossetie, haoni njia nyingine mbali na kujibu kwa kutumia sheria za kimataifa.
Hali ya matumaini ilishuhudiwa baada ya kufikiwa makubaliano ya kimataifa jijini Geneva Uswisi, na sasa mvutano unaibuka upya kati ya Urusi na mataifa ya magharibi.
Hayo yakijiri, jeshi na polisi vya Ukraine vimerejesha ofisi za manispa ya jiji la Mariupol kwenye himaya ya serikali, amesema waziri wa mambo ya ndani wa Ukraine, akibaini kwamba jengo hilo lilikua likishikiliwa kwa majuma kadhaa na wanaharakati wanaounga mkono kujitenga kwa eneo la mahariki mwa Ukraine.
Wanaharakati wanaunga mkono kujitenga kwa eneo la mashariki mwa Ukraine wakilinda jengo la serikali la mji wa Donetsk, aprili 21..REUTERS/Marko Djurica
“Ofisi za manispa ya jiji la Mariupol zimekombolewa na ofisi hizo zinaendesha shughuli zake kama kawaida”, Arsen Avakov ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook.
Mji huo unaopatikana kusini mashariki mwa Ukraine una watu wapatao 500.000