|
Pichani ni Morogoro, siku ya kwanza ya mgomo wa madereva. Inanikumbusha miaka ya 80 katikati kabla ya ujio wa daladala. Kulikuwa na shida kubwa ya usafiri dar. Serikali ikaruhusu kuingiza nchini magari ya wazi kwa ushuru mdogo. Watanzania wengi waliokuwa diaspora na hata waliokuwa wakirudi nchini walikuja na pickups zao.Picha na Mjengwa |
Nayanena haya huku leo hapa jijini Arusha kukiwa na mgomo wa wafanyabiashara hali inayosababisha maduka mengi kutokufunguliwa na watu kukwama kupata mahitaji yao huku swala hilo likiwa na adhari mabaya kiuchumi.
Sina dhumuni la kukupa habari za mgomo wa leo ila nikukumbushe pia siku chache zilizo pita madereva nchi nzima waligoma na kumekuwa na mfululizo wa migomo katika taifa hili.
Ukweli ni kwamba migomo husabishwa na kutokuelewana baina ya pande kuu mbili huku mara nyingi ikiwa ni mamlaka yenye dhamana husika ya usimamizi ikiwemo serikali.
Mfano mgomo wa madereva na wafanya bishara uosababishwa na TRA a mamlaka za juu za serikali kuto wasikiliza wahusika.
Ni ukweli usiofichika kwamba serikali yetu inatabia ya kudharau na kupuuzia malalamiko inayopewa kutoka kwa wafanyakizi ama wannchi kwa ujumla na huu ndio udhaifu ninao uzungumzia hapa.
Wito wangu kwako Rais Kikwete, hakikisha ya kwamba unafanya kazi kwa niaba ya wananchi wako na sio kundi au jamii fulani, Kwa mfano wapo watanzania wanaodai ya kwamba gharama wanazotozwa madereva ni mbinu ya serikali yako kujipatia fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa kisiasa mwaka huu ili chama chako kipite tena.
Nikukumbushe kwamba rais wa Marekani wa 16 Ndugu Abraham Linkon aliwahi kusema ya kwamba serikali nzuri ni ile inayofanya kazi kwa niaba ya wananchi walio wengi.