TAZAMA JINSI SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MAPINDUZI ZILIVYONOGA UWANJA WA TAIFA

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia wananchi wakati alipokuwa anaingi uwanja wa Uhuru leo katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar..Pembeni ni Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Joyce Banda wa Malawi katika sherehe za miaka 50 ya Muungano.Rais Banda kwa sasa ndiye mwenyekiti wa jumuiya ya uchumi kusini mwa Afrika SADC.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt.Mohamed Ali Shein wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya muungano.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Mfalme MswatiIII katika sherehe za miaka 50 ya Muungano zilizofanyika katika viwanja vya uhuru leo.


Rais dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Yoweri Kaguta Museveni katika sherehe za miaka 50 ya Muungano.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi katika maadhimisho ya hsrehe za miaka 50 ya Muungano.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Uhuru Kenyatta katika hsrehe za miaka 50 ya Muungano.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Mohamed Ali Shein na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis
Mwamunyange wakiwa na viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika kwenye sherehe za Miaka 50 ya Muungano katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo. Wengine toka kushoto ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi, Mfalme Mswati wa III

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal, Mfalme wa Lesotho na rais wa Malawi Dkt Joyce Banda. na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakiwa na viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika kwnyesherehe za Miaka 50 ya Muungano katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal, na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakishangilia kwa furaha wakati Makomandoo wakishuka kwa miavuli uwanjani kama inavyoonekana hapo chini. Mapicha ya kumwaga baadae kidoooogo....

Askari wa Miavumli akishuka
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company