|
Kiongozi wa UKAWA Mh. Mbowe |
|
Mwana chama wa UKAWA Tindu Lissu |
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba - Mwenyekiti CUF
Mwenyekiti Taifa wa chama cha upinzani cha CUF nchini Tanzania, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba, amesema kundi linalojiita Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) litaendelea kupigania haki ya Watanzania ya kupata katiba wanayoitaka na inayoakisi maoni yao waliyoyatoa mbele ya Tume ya Marekebisho ya Katiba. Kundi hilo linajumuisha wajumbe wa bunge maalum la katiba wanaopinga kile wanachodai ni ubabe wa chama tawala CCM kwenye bunge hilo. Akizungumza kwenye mahojiano maalum na idhaa hii, Prof. Lipumba ambaye pia ni mwanachama wa UKAWA amesema kundi hilo liko tayari kurejea bungeni iwapo CCM itaahidi kuheshimu rasimu ya katiba iliyoandaliwa na Tume ya jaji mustaafu, Joseph Warioba. Kundi hilo liliondoka kwenye vikao vya bunge maalum la Katiba wiki iliyopita likilalamikia kudharauliwa rasimu ya katiba. Wengi wa wajumbe wanaounda muungano wa UKAWA wanatoka katika vyama vya upinzani. Wajumbe hao wanasema kuna njama ya kupuuza vipengee muhimu vya rasimu ya katiba; jambo ambalo wameapa kulipinga kwa nguvu zote.