Boko Haram kuwauza wasichana waliotekwa


Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau

Kundi la wapiganaji wa kislamu nchini Nigeria la Boko Haram limesema linapanga kuwauza wasichana zaidi ya miambili ambao liliwateka nyara wiki tatu zilizopita

Hii ni baada ya kundi hilo hatimaye kukiri ndililo lililowateka wasichana hao baada ya kimya cha wiki tatu tangu kutekwa nyara kwao.
Kiongozi wa kundi hilo, Abubakar Shekau alituma kanda video ambapo alikiri kwa mara ya kwanza kuwa kundi hilo ndilo liliwateka nyara wasichana hoa.

Wasichana hao walitekwa kutoka shule moja iliyo kaskazini mashariki mwa nchi walipokuwa wajinadaa kwa mitihani yao.

Wakati huo mwanamke ambaye ni kiongozi wa maandamano nchini humo Naomi Mutah aliyekuwa amezuuiliwa na polisi kwa amri ya mke wa rais wa nchi hiyo Patience Jonathan ameachiwa huru.

Kumekuwa na shinikizo kwa serikali ya nchi hiyo kwamba haijafanya juhudi kubwa kuwaokoa wasichana hao.

Akizunguma kwa mara kwa kwaza kuhusu tukio hilpo rais wa Nigeria Goodluk Jonathan amesema kuwa atafanya awezalo kuwakoa wasichana hao.

Takriban watu 1500 wameuawa na kundi hilo mwaka huu likisema kuwa linapigana dhidi ya kile linachosema ni elimu ya kimagharabi.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company