Kerry akutana kwa mazungumzo na viongozi wa Umoja wa Afrika


John Kerry, waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani anakutana na viongozi wa Umoja wa Afrika.
REUTERS/Jason Reed Na RFI

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani John Kerry anakutana leo na viongozi wa Umoja wa Afrika kwenye makao makuu ya Umoja huo mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia, hatua ya kwanza ya ziara yake rasmi anayoifanya katika bara la Afrika.
       John Kerry atatatembelea baadhi ya mataifa ya kiafrika mkiwemo taifa changa la Sudani Kusini ambalo linakabiliwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe tangu desemba 15 mwaka 2013, baada ya viongozi vigogo wawili wa kundi la zamani la waasi la SPLA, rais Salva Kiir na makamu wake wa zamani aliye futwa kazi mwezi julai mwaka jana Riek Machar kutofautiana.

John Kerry amesema Marekani itahakikisha amani na utulivu vimerejea nchini Sudani Kusini.

Miili ya watu waliyouawa katika mapigano yaliyotokea hivi karibuni katika mji wa Bentiu, nchini Sudani Kusini.REUTERS/Emre Rende

Rais Salva Kiir amekua akiwatuhumu baadhi ya wapinzani wake akiwemo Riek Machar kupanga njama za kuipindua serikali yake, tuhuma ambazo zimekua zikikanushwa na Riek Machar akibaini kwamba ni njama za rais Salva Kiir za kutaka kuwakandamiza wapinzani wake. Machafuko ya Sudani Kusini yamesababisha maelfu ya raia kupoteza maisha na maelfu wengine kuyahama makaazi yao.

Sudani Kusini ni taifa changa duniani, ambalo lilijipatia uhuru wake julai mwaka 2011.

Marekani ilichangia kwa hali na mali ili Sudani Kusini ipate uhuru wake.
Baada ya kuondaka nchini Ethiopia, Kerry anatazamiwa atembelea nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Angola ambapo msemaji wa wizara ya mambo ya nje Jen Psaki amesema ni ziara inayolenga kuyahamasisha mataifa hayo kuhusu masuala ya amani na usalama hali kadhaklika haki za binadamu lakini pia namna ya kuimarisha demokrasia.

Ziara hiyo ya siku 6 itampelekea waziri Kerry kukutana na mashirika ya kiraia, makundi ya vijana, pamoja na asasi za kiraia.

Kerry, ambaye anatazamiwa kuhetimisha ziara yake na kurejea mjini Washington may 15, atajadili na wanaharakati wa mashirika ya kiraia ,viongozi ambao ni vijana barani Afrika kuhusu hatma ya bara la Afrika, kuendeleza biashara, kuwekeza pamoja na ushirikiano katika masuala ya maendeleo barani Afrika
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company