MRENO Jose Mourinho atakuwa kocha wa nne Chelsea chini ya umiliki wa Mrusi, Roman Abramovich kumaliza msimu bila taji – watatu waliomtangulia wote walifukuzwa.
Bilionea huyo Mrusi amekuwa cha msalie mtume kwa walimu wasiompa mataji katika uwekezaji wake Stamford Bridge.
Claudio Ranieri alikuwa wa kwanza kufukuzwa baada ya kukosa taji, Mtaliano huyo akifukuzwa hata kabla ya kumaliza mwaka mwaka ambao Abramovich aliingia 2004. The Blues ilimaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.
Wenzake wote walifukuzwa: Carlo Ancelotti (juu kushoto), Claudio Ranieri (juu kulia) na Avram Grant (chini kulia) wote walifukuzwa kwa kumaliza mwaka bila taji. Moutinho chini kulia atapona?
Miaka minne baadaye alifuatia Avram Grant alipopigwa chini kwa kumaliza msimu bila taji, licha ya kuifikisha timu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambako kukosa penalti kwa John Terry kulimuangusha Muisrael huyo katika mechi na Manchester United mjini Moscow. Chelsea imaliza ya pili tena na Grant akafukuzwa.
Kisha, mwaka 2011, Carlo Ancelotti – licha ya kutwaa mataji mawili ya nyumbani miezi 12 iliyotangulia, alikuwa kocha wa tatu kufukuzwa na Abramovich.
Hata Rafa Benitez, ambaye aliipa Chelsea taji la Europa League, naye alipigwa chini mwishoni mwa msimu uliopita na sasa Mourinho ambaye yupo kazini, ametolewa katika Ligi ya Mabingwa Nusu Fainali na kwenye ubingwa wa Ligi Kuu inaelekea kuzidiwa kete na Liverpool na Manchester City.
MAKOCHA WA CHELSEA CHINI YA ROMAN...
2003/04 – Hakutwaa taji
Claudio Ranieri (Mei akafukuzwa)
2004/05 – Ligi Kuu na Kombe la Ligi
Jose Mourinho
2005/06 – Ligi Kuu
Jose Mourinho
2006/07 – Kombe la FA Cup, Kombe la Ligi
Jose Mourinho
2007/08 – Hakutwaa taji
Jose Mourinho (Septemba akafukuzwa) Avram Grant (Mei, akafukuzwa)
2008/09 – Kombe la FA
Luiz Felipe Scolari (Februari akafukzwa), Guus Hiddink (Mei akaondoka akaachia ukocha wa muda
2009/10 – Ligi Kuu, Kombe la FA
Carlo Ancelotti
2010/11 – Hakutwaa taji
Carlo Ancelotti (Mei, akafukuzwa)
2011/12 – Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la FA
Andre Villas-Boas (Machi akafukuzwa Roberto Di Matteo
2012/13 – Europa League
Roberto Di Matteo (Novemba akafukuzwa), Rafa Benitez (Mei, alimaliza mkataba wake wa muda mfupi
2013/14 – Hakutwaa taji
Jose Mourinho (je, atachukua taji?)
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago