NI SEVILLA BINGWA EUROPA LEAGUE 2014, NDOO ZOTE ZA UEFA ZABAKI HISPANIA

SEVILLA ya Hispania imetwaa ubingwa wa Europa League baada ya kuifunga Benfica ya Ureno kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120.
Mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Juventus, mjini Torino, Italia ulikuwa wa kawaida na timu zote zilicheza kwa tahadhari, hali iliyosababisha hata mashambulizi yawe machache.

Wafalme; Wachezaji wa Sevilla wakiwa na taji la Europa League baada ya kuifunga kwa penalti Benfica


Fainali kweli: Jose Antonio Reyes wa Sevilla akichuana na Rodrigo Moreno na Ruben Amorim wa Benfica katika Fainali ya Europa League usiku huu Uwanja wa Juventus mjini Torino.




Shujaa; Kipa Beto akipangua penalti ya Rodrigo
Bacca, M’Bia, Coke na Gameiro ndiyo walifunga penalti za Sevilla, wakati wa Cardozo na Rodrigo walikosa za Benfica, huku Lima na Luisao wakifunga.
Sifa zimuendee kipa Mreno wa Sevilla Antonio Alberto Bastos Pimparel aliyewazuilia ndugu zake leo na kucheza penalti moja ya Rodrigo, wakati ya Cardozo ilikwenda nje.
Ushindi wa Sevilla unamaanisha mataji yote ya klabu ya UEFA msimu huu yamebaki Hispania, kwani Atletico Madrid na Real Madrid nazo zitakutana katika Fainali ya Ligi ya Mabingwa baadaye mwezi huu nchini Ureno.
Vikosi vilikuwa, Sevilla: Beto, Coke, Pareja, Fazio, Moreno, Mbia, Carrico, Reyes/Marin dk78/Gameiro dk104, Rakitic, Vitolo/Diogo Figueiras dk110 na Bacca.
Benfica: Oblak, Maxi Pereira, Luisao, Garay, Siqueira/Cardozo dk99, Ruben Amorim, Gomes, Gaitan/Ivan Calvaleiro dk119, Sulejmani/Andre Almeida dk25, Lima na Rodrigo.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company