Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akitoa maneno ya utangulizi kwa Waheshimiwa Wabunge wakati wa semina ya wabunge wote kwa ajili ya uwasilishwaji wa mapendekezo ya mfumo wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2014/2015.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Uhusiano Mhe. Steven Wazira akiwasilisha mwelekeo wa hali ya uchumi kwa mwaka 2014/2015 kwa waheshimiwa wabunge
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum akiwasilisha Mapendekezo ya Mfumo wa Mapato na Matumizi ya serikali kwa mwaka wa fedha 2014/15 kwa Waheshimiwa Wabunge.
Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilila akisikiliza kwa makini hotuna ya Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum akiwasilisha Mapendekezo ya Mfumo wa Mapato na Matumizi ya serikali kwa mwaka wa fedha 2014/15 kwa Waheshimiwa Wabunge.
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda, Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Uhusiano Mhe. Steven Wazira wakipitia nyaraka mbalimbali wakati Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akitoa maneno ya utangulizi kwa Waheshimiwa Wabunge wakati wa semina ya wabunge wote kwa ajili ya uwasilishwaji wa mapendekezo ya mfumo wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2014/2015.
Wabunge wakifuatilia hotuba kwa makini.
Watendaji wa Wizara ya Fedha wakimsikiliza Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum. Picha na Owen Mwandumbya
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago