Washtakiwa hao ni Alune Kasililika (38), Neema Batchu (26) wafanyakazi wa benk hiyo, Kakame Julius (38), Iddy Khamis (32), Sezary Msolopa (31), Boniphace Muumba (29) na Ruth Macha (30) wafanyabiashara.
Wakisomewa mashitaka yao mbele ya hakimu Mkazi, Nyigulila Mwaseba ambapo Wakili wa Serikali Tumaini kweka akisaidiana Mwanaamina Kombakono walidai kuwa wastuhumiwa hao wanakabiliwa na mashtaka mawili.
Aliieleza mahakama kuwa katika tarehe tofauti zisizo fahamika washtakiwa wakiwa ndani ya jiji la Dar es Salaam walikula njama kwa nia ya kutenda kosa la wizi.
Katika shtaka la pili washtakiwa wanadaiwa kuwa Aprili 15 mwaka huu, wakiwa katika benki hiyo tawi la Kinondoni, Dar es Salaam waliiba fedha tasilimu sh.
milioni 390.2, Dola za Marekani 55, 000 na Euro 2150 mali ya Barclays.
Hata hivyo, ilidaiwa kuwa kabla ya kufanya wizi huo walimtishia kwa silaha Anifah Ahmad na Anna Tegete ambao ni wafanyakazi wa benki hiyo ili kuweza
kujipatia na kumiliki fedha hizo.
Baada ya washtakiwa hao kusomewa mashtaka hayo walikana kuhiska na tukio hilo, ambapo wakili Kweka alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika
wanaomba tarehe nyingine ya kutajwa.
Hakimu Mwaseba alisema kwa mujibu wa sheria shtaka la pili halina dhamana, kwa hiyo washtakiwa watakuwa chini ya ulinzi na kupelekwa gerezani hadi Mei 15 kesi hiyo itakapotajwa.
mwaka huu.
Katika tukio hilo ilielezwa kuwa majambazi hao walifika katika benki hiyo Aprili 15, mwaka huu, saa 9:00 mchana wakiwa na magari mawili na bunduki aina ya SMG pamoja na bastola, kisha waliingia ndani ya benki hiyo na kupora fedha walizotoka nazo kwenye mfuko na kukimbia nazo kwa kutumia pikipiki.
Hivi karibuni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Sulemain Kova akizungumza tukio hilo alisema kuwa wamegundua baadhi ya matukio ya wizi wa fedha unafanywa na wafanyakazi wa benki.
Alisema katika wizi huo, robo tatu ya fedha zote zilizoibwa zilichukuliwa siku moja kabla ya tukio linalodaiwa kutengenezwa la wizi, kwa lengo la kuficha wizi huo na kwamba kulikuwa na vikao mbalimbali vya maandalizi ya kufanikisha tukio hilo.
Alisema Aprili 15, mwaka huu siku ambayo wizi huo unatajwa kufanyika, kilichotokea ni tukio la kukamilisha njama hizo.
“Tukio hili lilileta utata tangu mwanzo tulipokwenda kukagua eneo la tukio, kwani siku moja kabla, yaani Aprili 14, gari la kubebea fedha kupeleka Benki Kuu lilifika katika tawi hilo kama ilivyo kawaida lakini fedha hazikutolewa kumbe ilikuwa ni mkakati uliowekwa kufanikisha wizi huo.”
CHANZO LUKAZA