Shirikisho la Kandanda la Dunia, FIFA, limeionya Nigeria kwamba itatolewa katika kandanda ya kimataifa iwapo serikali haitalirejesha tena shirika la kandanda la Nigeria, Nigerian Football Federation, ifikapo Jumaane juma lijalo.
Siku ya Alkhamisi serikali iliifuta Nigerian Football Federation na Ijumaa rais wa shirika hilo alikamatwa baada ya kurudi kutoka Kombe la Dunia
Nigeria ilishindwa kwenye mechi na Ufaransa na hivo kukosa kuingia katika robo-fainali.
FIFA imesema imetiwa wasi-wasi na hatua ya serikali ya Nigeria dhidi ya chama cha kandanda cha nchi hiyo.
Kanuni za FIFA zinaeleza wazi kuwa wanachama wake lazima waruhusiwe kufanya kazi yao bila ya kuingiliwa kati na serikali.
Wakuu wa Nigeria wamekifuta chama cha kandanda cha taifa na piya kumkamata rais wa chama; na waziri wa michezo amemteua mkurugenzi wake kuongoza chama hicho.
Haijulikani sababu ya serikali ya Nigeria kufanya hivyo.
Lakini iwapo serikali haitabadili uamuzi wake basi Nigeria haitaweza kushiriki katika mechi za kimataifa, mazoezi na kadhalika.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago