Kituo cha Televisheni ta Katalunya kimeripoti kwamba ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 63 imekubaliwa na Suarez atasaini Mkataba wa miaka mitano, ambao utamfanya awe mchezaji wa nne kulipwa fedha nyingi baada ya Lionel Messi, Neymar na Andres Iniesta.
Liverpool wanaendelea na mipango ya kutaka kumsajili Alexis Sanchez wa Barcelona azibe pengo la Suarez.

Dili limetimia: Luis Suarez sasa yuko njiani kuhamia Barcelona.
Arsenal inabakia kuwa chaguo la kwanza la Sanchez, lakini Manchester City na United zimeonyesha pia nia ya kuitaka huduma yake sawa na Juventus.
Sanchez atasafiri kutoka Santiago, Chile hadi Barcelona nchini Hispania kujadili ofa hizo mezani. Barcelona inatarajiwa kutoa tamko rasmi juu ya Suarez kesho.