Wahudumu wa afya huko Magharibi mwa Afrika wakitoa huduma kwa waathirika wa virus vya Ebola
AFP PHOTO / SEYLLOU
Na RFI
Idadi kubwa ya ripoti mpya za maambukizi ya virusi vya Ebola imetajwa huko Sierra Leone na Liberia ambapo kumearifiwa vifo 19 kutokea ndani ya siku tatu za juma hili,shirika la afya duniani WHO limearifu.
Idadi hiyo inaonesha kwamba ni harakati dhidi ya muda wa kudhibiti ugonjwa huo huko Sierra Leone, wameeleza madaktari wasio na mipaka.
Kwa ujumla kumetokea vifo 539 huko Afrika Magharibi tangu kutokea kwa ugonjwa huo katika taifa jirani la gine mnamo mwezi wa pili.
Viongozi katika ukanda huo wamekubaliana kuchangisha fedha kwa ajili ya kukabiliana na kuenea kwa ugonjwa huo.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago