Mshambuliaji staa wa timu ya Chelsea, Didier Drogba ameamua kujenga clinic ya kwanza katika Jiji la Abijan, Ivory Coast kwa lengo la kusaidia jamii yake chini ya The Didier Drogba Foundation.
Hii ni ya kwanza kati ya zile tano ambazo Secretary ya Foundation hiyo, Guy Roland Tanoh aliahidi kwamba wamejipanga kuzijenga ndani ya Ivory Coast kwa ajili ya kusogeza huduma hiyo kwa watu.
Didier ameoanga kuchezesha mechi London Feb 18 ili kuchangisha pesa nyingine ambazo zitasaidia kukamilisha ahadi yake ya ujenzi wa clinic hizo.
Roland alisema Didier aliona ni bora kujenga clinic hizo tano nyumbani kwao kuliko kujenga hospitali moja kubwa kwa kuwa hospitali moja isingeweza kuhudumia maeneo mbalimbali na kwa wingi kama ambayo clinic zinaweza kuhudumia watu hao.