Kumekuwa na desuri katika mataifa mengi duniani ya kusomesha madereva pekee na kuwaacha wasaidizi wao hali ambayo mimi kwa nguvu zote ninaipinga na kuiona kuwa hailengi kuondoa kero na matatizo yalipo baranbariani au kwenye usafiri wa umma.Mimi huwa ninaamini ya kwamba hakuna kazi au fani yoyote ile inayohusisha maisha ama masilai ya jamii isoyohitaji elimu ,
Naongea haya kwani leo asubuhi nikiwa katika usafiri wa umma kondakita alitaka kumpakia abiria angali gari lipo barabarani ila dereva wake akamkemea na kumwambia kuwa hauni gari lipo barabarani ngoja kwanza nipaki gari.
Nikatafakari kwa kina nikafahamu kuwa, kumbe madereva wamesomeshwa na wakakubali kusoma kwa hiyo wanafahamu maadili ya kazi yao vyema.
Ila makondakita hawajapelewa shle na wala hakuna sheria au kibali maalumu kwao kinachowataka wafanye hivyo.
Kwa hiyo naitaka serikali iwapeleke makondakita wote waende shule, kwani wakifanya hivyo watasaidia kujua maadili yao hata katika uvaaji kwani wengi wao wanavaa mavazi yasiokuwa na maadili na lugha zao pia sio njema.kwa hiyo shule itawapa maadili yao yote ikiwemo kuwafundisha sheria zote za usalama barabarani.