Ndege za kijeshi za Kenya zimeshambulia maeneo ya wapiganaji wa kundi la Alshabaab katika taifa jirani la Somalia ,msemaji wa jeshi ameiambia BBC.
Ndege hizo zililenga maeneo mawili ya jimbo la Gedo,linalotumiwa na wapiganaji hao kuvuka na kuingia Kenya, msemaji huyo ameongeza.
Maeneo hayo mawili hutumiwa na wapiganaji hao kupanga mshambulizi nchini Kenya.
Wanajeshi wa AMISOM walitarajiwa kupeleka wanajeshi wao katika eneo hilo la Gedo lakini hadi sasa hawajafanya hivyo.
Hili ni shambulio la kwanza la Kenya kwa shambulizi la alshabaab ambalo lilisababisha mauaji ya watu 148 katika chuo kikuu cha Garissa wiki iliopita.Amisom
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameapa kujibu shambulizi hilo kwa njia mbaya zaidi.
Msemaji wa jeshi la Kenya David Obonyo ameiambia BBC kwamba Jeshi la Kenya lilijibu vitisho kwa kutekeleza mashambulizi ya angani siku ya jumapili usiku katika eneo hilo.
Hakuna maelezo zaidi ya oparesheni hiyo yaliotolewa.
CHANZO BBC SWAHILI