Viongozi wa dunia wanahudhuria kumbukumbu ya miaka 100 ya mauaji ya Waarmenia milioni 1.5 yaliofanywa na Waturuki wakati wa himaya ya Ottoman.
Mauaji hayo yaliyotokea wakati wa vita vikuu vya kwanza vya dunia kwa kiasi kikubwa yanachukuliwa kama ni mauaji ya kimbari. Uturuki ya kisasa ambayo imechukuwa nafasi ya himaya ya Ottoman inapinga vikali mauaji hayo kuitwa kuwa ya halaiki.Rais Vladimir Putin wa Urusi na mwenzake wa Ufaransa Francois Hollande pamoja na viongozi wengine wa dunia kila mmoja ameweka waridi la rangi ya njano katika jengo la kumbukumbu kwenye mji mkuu wa Yerevan.
Akizungumza hapo jana usiku katika misa ya kumbukumbu ya mauaji hayo Rais Joachim Gauck wa Ujerumani kwa mara ya kwanza ametamka kwamba mauaji hayo yalikuwa ya kimbari.Bunge la Ujerumani leo linajadili mauaji hayo na linategemewa kutowa tamko rasmi.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago