Mitandao ya kijamii
Utawala nchini Burundi umekata mawasiliano ya mitandao ya kijamii kupitia kwa simu ya mkononi mawasiliano ambayo wamekuwa wakitumia kupanga maandamano ya kumpinga rais Pierre Nkurunziza.
Mamia ya waandamanaji wako barabarani kwenye mji mkuu wa Buruni ,Bujumbura kwa siku ya nne ya ghasia kutokana na uamuzi wa rais kwa kuwania muhula wa tatu.
Maandamano Burundi
Mwandishi wa BBC nchini Burundi anasema aliwaona waandamanaji katika eneo la Musaga wakiinua mikono kuwaonyesha polisi kuwa hawakuwa wamejihami.
Wanasema kuwa wanazuiliwa kuondoka na kuwa chakula hakifiki eneo hilo.