Mkuu wa shule alilia bweni kupunguza mimba

Mwandishi wetu
SHULE ya Sekondari ya Zimanimoto iliyopo Kata ya Ruvuma Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, inakabiliwa na chanagamoto ya ukosefu wa bweni la wasichana, jambo ambalo linachangia wanafunzi wa kupata mimba.

Hayo yalielezwa na mkuu wa shule hiyo, Kandidus Kowero, mbele ya meneja wa Benki ya Posta tawi la Songea ,Joseph Shirima, ambaye alienda kutoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri mitihani ya kidato cha nne kwa mwaka wa 2014.

Kowero alisema kuwa licha ya shule hiyo ambayo ni ya kata kuonyesha kuwa inauwezo wa kufanya vizuri katika mihani yake lakini bado kumekuwepo na changamoto za ukosefu wa nyumba za walimu pamoja bweni la wasichana.


“Mwaka jana kuna mwanafunzi wa kike amefanya mitihani akiwa na ujauzito wa miezi nane na akapata alama ya pasi,” alisema.

Alisema kuwa kwa hali kijografia ya mahali ilipojengwa shule hiyo ni sehemu nzuri ya kusomea lakini inatakiwa kuwa na bweni la wasichana kwa kuwa wanafunzi waliowengi wanatoka umbali mrefu hivyo baadhi yao hukutana na vishawishi.

Mkuu huyo alifafanua kuwa kwa msimu wa mwaka jana 2014 wanafuzi 46 waliweza kufanya mtihani wa kidato cha nne katika hao wanafunzi waliofanya vizuri ni wawili.

Kwa upande wake Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Songea , Joseph Shirima wakati akiwakabidhi zawadi ya Sh 600, 000 kwa wanafunzi wawili waliopata alama za ufaulu alisema anatekeleza ahadi ambayo aliwaahidi wanafunzi hao siku ya mahafali.

Shirima alisema kuwa sekondaeri za kata hazitakiwi kubezwa kwa kuwa zinauwezo wa wanafunzi wake kufanya vizuri kama jamii itaungana pamoja kutatua kero ambazo huwa zinajitokeza kwenye shule hizo ikiwemo kama suala la bweni kwa wanafunzi wa kike.
CHANZO MPEKUZI
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company