NAMNA YA KUMSHITAKI DAKTARI ALIYESABABISHA MADHARA AU KIFO KWA MGONJWA.

Na Bashir Yakub.

Wako watu wengi wameathirika kutokana na matendo yanayotokana na uzembe,kutojali au makusudi ya madaktari. Wapo waliopata vilema vya muda kutokana na uzembe huo, wapo waliopata vilema vya maisha na wapo waliouliwa na madaktari hawa hawa.

Ajabu ni kuwa ukifanya tathmini ya haraka utaona kuwa watu wote waliopata madhila kutoka kwa madaktari huhusisha madaktari wa serikali na katika hospitali za serikali. Si rahisi kukuta jambo la ajabu la kitabibu limehusisha hospitali binafsi. Swali langu ni kuwa, ewe Mtanzania daktari amekusababishia tatizo iwe ugonjwa wa kudumu, ulemavu wa muda au wa kudumu, au hata kifo cha ndugu au jamaa, umechukua hatua gani baada ya tukio hilo ?. Umekaa kimya ukiwa umeridhika au umekaa kimya kwakuwa hujui la kufanya ?.

1.INARUHUSIWA KUMSHITAKI DAKTARI KWA KUSABABISHA
MADHARA KWA MGONJWA WAKATI WA TIBA.
Wapo wanaodhani kuwa madaktari hawashitakiwi kwa kutomhudumia vyema mgonjwa. Hili si kweli daktari ni mtumishi sawa na watumishi wengine na kosa lolote la uzembe, kutojali au makusudi analofanya na kusababisha madhara kwa mgonjwa sheria inaruhusu kumchukulia hatua daktari huyo. Sawa na mtumishi mwingine akitenda kosa kazini anaadhibiwa ndivyo ilivyo kwa madaktari pia. Kwa mujibu wa sheria daktari amepewa wajibu wa hali ya juu kuhakikisha anatumia taaluma yake, weledi na uadilifu katika kutoa huduma ya tiba na kuepuka kabisa hatua au namna yoyote inayoweza kuleta madhara kwa mgonjwa.

Takwa hili kwa daktari ni takwa la kisheria na wala si hiyari. Kwa hiyo watu waelewe kuwa suala la daktari kutoa matibabu kwa umakini ni lazima. Kitu kikiwa lazima (mandatory) katika sheria maana yake ni kuwa kutofanyika kwake hutoa haki ya mtendewa kushitaki. Hivyo ndivyo ilivyo kwa madaktari. Kwa namna yoyote anapokosa umakini katika kutoa tiba basi ni ruhusa kwa mtendewa kushitaki.

KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company