Pakistan:Wanamgambo kifungoni

Malala Yousafzai alipigwa risasi ya kichwa na Wanamgambo wa Taliban

Mahakama moja ya Pakistan imewahukumu kifungo cha maisha wanamgambo 10 waliopatikana na hatia ya kuhusika katika tukio la miaka 3 iliyopita ,la kumshambulia kwa kumpiga risasi mwanaharakati wa kutetea haki za watoto, msichana Malala Yousafzai.

Wakati wa shambulio hilo ambapo alijeruhiwa vibaya sana baada ya kupigwa risasi ya kichwa , alikuwa na umri wa miaka 15 pekee .

Alilengwa na wanamgambo wa Taliban wa huko Pakistani kwa kuonekana kuwa mstari wa mbele kupigia kampeni ya kuendeleza elimu kwa wasichana.

Mwaka jana msichana Malala Yousafzai alitunukiwa tuzo la kimataifa la Nobel akiwa mshindi mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kushinda tuzo hilo la amani Nobel Peace Prize.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company