Wahamiaji wakionekana wamebanana kwenye manwari ya jeshi la majini la Utaliana
Takriban wahamiaji 700 walokuwa wanajaribu kusarfiri kwa boti kutafuta maisha bora Ulaya wanahofiwa wamefariki pale boti yao ilipozama nje ya pwani ya Libya.
Maafisa wa usalama wanasema watu 28 wameokolewa na miili 24 imegunduliwa lakini mamia ya watu hawajapatikana bado katika ajali inayosemekana ni mbaya kabisa ya kutoweka kwa wahamiaji katika bahari ya Mediterranean.
Meli ilizama km 193 kusini mwa kisiwa cha Utaliana cha Lampadusa, wakati inaaminika wahamiaji walikwenda upnde mmoja wa boti wakati meli kubwa ya mizigo ilikuwa inapita karibu yao.
Viongozi wa Ulaya wametoa wito wa kuchukuliwa hatua za mara moja kutanzua mzozo wa wahamiaji wakati maelfu ya watu kutoka Afrika na Mashariki ya Kati wanajaribu kukimbia kutokana na ufukara, vita na vurugu la kisiasa linalosababisha ukosefu wa usalama katika nchi za kiarabu. Watu hao wanasongamana katika boti na kujaribu kuvuka bahari ya Mediterranean , kuelekea hasa Utaliana.
Mkuu wa masuala ya Kigeni ya Umoja wa Ulaya Federica Mogherini anasema “ Tumesema mara nyingi sana, isipate kutokea tena, huu ni wakati wa Umoja wa Ulaya kukabiliana na maafa haya bila ya kuchelewa.”
Waziri Mkuu wa Utaliana Matteo Renzi anasema vidadi ya vifo bila shaka inatazamiwa kuongezeka akiuliza, “inakuwaje tunashuhudia maafa haya kila siku?”
Rais Francois Hollande wa Ufaransa anasema ni lazima kwa maafisa kupambana na biashara haramu ya kusafirisha binadamu inyosababisha vifo vya zaidi ya watu elfu nne katika bahari ya Mediterranean wanaojaribu kutafuta maisha bora Ulaya.
Maelfu ya wahamiaji wengi wao kutoka maeneo yenye vita Afrika na Mashariki ya Kati wanafanya safari ya hatari kubwa kuvuka bahari ya Mediterrean kwa matumaini ya kuwasili Ulaya.
Siku ya Ijuma Rais Barack Obama na mgeni wake Waziri Mkuu wa Utaliana Matteo Rnezi walijadili suala la wahamiuaji wakati wa cmazungumzo yao hapa Washington.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago