Waziri Mkuu wa zamani Tony Blair
Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair amejiuzulu nafasi ya ujumbe wa umoja wa kimataifa katika kamati unaoshughulikia usuluhishi wa mgogoro wa Mashariki ya kati Quartet, unaohusisha nchi ya Israel na Palestina nafasi ambayo ameitumikia kwa kipindi cha miaka nane.
Vyanzo vya habari vilivyokaribu na Blair vinasema ataendelea kuwepo akijihusisha na baadhi ya shughuli na eneo hilo. Watoa habari hao wanasema kuwa waziri mkuu huyo anaamini kuwa mtazamo mpya unahitajika. Lakini wakosoaji wanasema Blair alipambana katika jukumu ambalo lilikuwa na mipaka katika maendeleo ya kiuchumi na ameshindwa kuleta matokeo chanya. Afisa mmoja wa Palestina amemlaumu Blair kwa kufanya kazi ili kuwaridhisha waisrael na Marekani. Umoja huo unaundwa na UN, EU nchi ya Marekani na Urusi.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
6 years ago

