Muandamanaji aficha uso wake kwa majani Burundi.
Kanisa katoliki la Burundi limesema kuwa linajiondoa katika kuunga mkono uchaguzi unaotarajiwa nchini humo baada ya majuma kadhaa ya michafuko. Kanisa hilo limetoa taarifa Jumanne likisema kuwa limewasihi makisisi wote wanaohudumu kwenye tume za uchaguzi kujiondoa kwenye nyadhifa zao.
Jumatano serikali ya Burundi ilitoa wito kwa wa rundi kutoa michango yao ili kufadhili uchaguzi baada ya wafadhili wa kigeni kutishia kutofadhili iwapo rais Nkurunziza ataendelea na mpango wa kuwania wadhifa kwa muhula wa tatu.
Tangazo la rais mwishoni mwa mwezi uliopita limechochea ghasia na taharuki za kisiasa kwa majuma kadhaa ambapo zaidi ya watu 20 wamekufa na zaidi ya 500 kujeruhiwa kwenye makabiliano na polisi.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
6 years ago

