Merkel ataka suluhu kwa mazungumzo

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kushoto, na Rais wa Urus Vladmir Putin wakiwa katika mkutano na waandishi habari huko Kremlin,Moscow,Urusi

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel,amesema kwamba historia inatoa funzo la umuhimu wa kupata suluhu ya migogoro ya aina mbali mbali kwa njia ya majadiliano.

Akiongea na waandishi wa habari Kansela Angela Merkel alisisitiza umuhimu wa mkataba wa amani kuhusu Ukraine kuandaliwa.

Mapema kiongozi huyo wa Ujerumani aliweka shada la maua kama ishara ya kuwakumbuka wanajeshi wa nchi mbili hizo waliokufa katika vita vikuu vya pili vya dunia,kuadhimisha siku ambayo majeshi ya Ujerumani yaliposalimu amri kwa vikosi vya majeshi ya washirika miaka sabini iliyopita.

Katika mazungumzo baina yake na Rais Vladimir Putin,Merkel alionya hatua ambazo vikosi vya majeshi ya Urusi dhidi ya Ukraine na kuweka bayana kwamba hatua hizo zinahatarisha usalama wa umoja wa Ulaya.

Naye kiongozi wa Urusi Vladmir, amesema kwamba makubaliano ya amani yaliyofikiwa Belarus mnamo mwezi wa pili mwaka huu yanaendelea vizuri.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company