Mkutano wa kikanda nchini Tanzania kutatua mgogoro wa Burundi

Polisi ikiwatawanya waandamanaji katika wilaya ya Buterere, kaskazini magharibi mwa jiji la Bujumbura, Mei 12 mwaka 2015.
REUTERS/Goran Tomasevic
Na RFI

Mkutano wa kikanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kutafutia suluhu mgogoro unaoendelea kushuhudiwa nchini Burundi unatazamiwa kufanyaka Jumatano wiki hii mjini Dar es Salaam , nchini Tanzania.

Mbali na Rais Nkurunziza, marais Paul Kagame wa Rwanda, Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya wanatazamiwa kushiriki katika mkutano huo.

Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pia amealikwa katika mkutano huo, ikiwa ni pamoja na makamu wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.

Wiki moja iliyopita waziri wa mambo ya nje wa Tanzania, Bernard Membe alitoa tangazo fupi katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa maandalizi wa mkutano wa marais wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, mjini Bujumbura, nchini Burundi. Waziri Membe alisema kuwa masuala mawili makuu yatakaojadiliwa katika mkutano huo wa marais ni " usalama nchini Burundi " na "tatizo la wakimbizi ".

Hata hivyo, waziri Membe hakutaja sababu ya mgogoro wa kisiasa, ambayo ni mgombea kwa muhula wa tatu rais aliyeko madarakani Pierre Nkurunziza. Kwa maoni ya wanadiplomasia kadhaa, haina haja ya kusubiri mkutano huu kuamua wazi juu ya uhalali au la ya muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza.

Kwanza kwa sababu ni suala la uhuru wa nchi na sera za ndani. Marais wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wanasita kuingilia wazi masuala ya majirani zao. " Itakua ngumu zaidi katika kutafutia ufumbuzi mgogoro wa Burundi, wakati ambapo wengi miongoni mwa marais hawa wenyewe wanatafuta mbinu za kuendelea kusalia madarakani", amesema mdadisi mmoja kutoka tanzania.

Tanzania inaweza kutafuta njia mbili ili kutafutia ufumbuzi mgogoro unaoendelea kushuhudiwa Burundi: kuanzishwa kwa mazungumzo kati ya Nkurunziza na upinzani na uchaguzi kuahirishwa.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company