Mvutano wa kisiasa waendelea Makedonia

Waziri mkuu wa Makedonia Nikola Gruevski mbele ya wafuasi wake Mei 18 mwaka 2015, katika mji wa Skopje.
REUTERS/Marko Djurica
Na RFI

Mvutano wa kisiasa unaendelea kati ya serikali ya Makedonia na upinzani. Maima ya maelfu ya watu wameandamana Jumatatu jioni katika mji wa Skopje wakimuunga mkono waziri mkuu Nikola Gruevski.
     Maandamano hayo yaliyoitishwa na serikali yamefanyika siku moja baada ya maandamano mengine makubwa yaliyoitishwa na upinzani ukiomba kujiuzulu kwa Nikola Gruevski. Wafuasi wa upinzani wameendelea kupiga kambi Jumatatu jioni wiki hii mbele ya makao makuu ya serikali.

Kiongozi mkuu wa upinzani Zoran Zaev, amefichua rekodi ya mazungumzo ambayo ilionekana kuonyesha udhibiti wa karibu wa viongozi juu ya waandishi wa habari, mahakimu, na juu ya taratibu za uchaguzi.Hatua hizo za uchunguzi zinasadikiwa kulenga watu wapatao 20,000. Wapinzani lakini pia washirika wa utawala. Waziri mkuu hakukana usahihi wa yaliyomo katika rekodi hiyo, lakini amekanusha kuwa na udhibiti juuu ya watu hao.

Kiongozi huyo wa upinzani, tangu wakati huo alifuatiliwa kwa kosa la “ unyanyasaji dhidi ya serikali “. Lakini wengi miongoni mwa raia wanampinga waziri mkuu wakitaka ajiuzulu. Zaidi ya mahema thelathini yamejengwa tangu Jumapili mwishoni mwa juma lililopita mbele ya makao makuu ya serikali.

Hata hivyo waziri mkuu Nikola Gruevski haonekani hata kidogo kuwa ataachia ngazi. Nikola Gruevski alirejea madarakani kwa muhula mmoja wa miaka minne wakati wa uchaguzi wa wabunge uliyofanyika mwezi Aprili 2014. huku akisema kuwa hana nia ya kujiuzulu.

Wakati huo huo mazungumzo yameanzishwa chini ya mwumvuli wa Umoja wa Ulaya na Marekani ili kutafutia suluhu mzozo huo wa kisiasa unaoendelea nchini Makedonia.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company