Rushwa :Wanajeshi washikiliwa Malawi

Jenerali Odillo alikua Kiongozi wa Jeshi mpaka alipofukuzwa na Rais Mutharika mwaka 2014

Mkuu wa majeshi wa zamani nchini Malawi amekamatwa akihusishwa na vitendo vya rushwa vya mamilioni ya dola.

Jenerali Henry Odillo na aliyekuwa makamu wake Luteni Kanali Clement Kafuwa, wanashutumiwa kupanga mkataba wa kuingizwa kwa vifaa vya kijeshi nchini Malawi, vifaa ambavyo havikuwasilishwa nchini humo.

Taasisi ya kuzuia rushwa nchini Malawi, ACB inawashikilia Viongozi hao wa kijeshi wa zamani ikiwa ni sehemu ya uchunguzi unaofanywa ndani ya Serikali kuhusu kashfa ijulikanayo kama ''Cashgate''.

Viongozi hao wa kijeshi hawakuzungumzia lolote kuhusu shutma hizo.

Mwandishi wa BBC mjini Blantyre amesema watumishi kadhaa wa umma wameshutumiwa kuhusika kwenye kashfa ya ''Cashgate''

Kashfa hiyo imebainisha kuwepo kwa matumizi ya fedha bila huduma kutolewa.Maandamano yalifanyika baada ya kubainika kwa kashfa ya ''Cashgate''

Taarifa inasema kuwa Jenerali Odillo na Luteni kanali Clement Kafuwa wanakabiliwa na mashtaka ya kutumia ofisi vibaya, uzembe wa afisa wa uma katika kuhifadhi fedha na biashara haramu ya fedha.

Uchunguzi umebaini kuwa Jeshi lililipa kiasi cha dola milioni 4.4 kwa ajili ya vifaa hewa.

Kashfa ya ''Cashgate'' ilijitokeza kwa uchache mwezi septemba mwaka 2013 baada ya jaribio la mauaji dhidi ya Mkurugenzi wa bajeti wa Wizara ya Fedha, Paul Mphwiyo.

Siku kadhaa kabla,Mtumishi mmoja wa Serikali alikutwa na zaidi ya Dola 300,000 kwenye gari lake.

Fedha zaidi zilizuiliwa kutoka mikononi mwa wafanyakazi wa Serikali walizokuwa wamezificha nyumbani na kwenye magari.

Nchi wahisani wa Malawi walizuia kiasi cha dola milioni150 kushinikiza uchunguzi zaidi kufanyika.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company