SNP yazoa viti 56 kati ya 59 Scotland

Kiongozi wa SNP haamini kilichofanyika Scotland

Chama ambacho kimewashangaza wengi katika uchaguzi mkuu wa Uingereza ni kile cha Scotland National Party The SNP.

Chama hicho ambacho kilichopata umaarufu haswa baada ya kura ya maoni ya kujitenga au kusalia katika muungano wa Uingereza kiliandikisha ushindi wa asilimia kubwa nchini Scotland.

SNP kimeshinda viti 56 kati ya viti 59.BBC ilikuwa imebashiri kuwa chama cha SNP kitashinda asilimia kubwa ya viti Scotland.

Chama ambacho kilikuwa na ushawishi mkubwa nchini humo cha Labour kimesalia na mbunge mmoja tu Scotland.

Wimbi la SNP lilikuwa kubwa kiasi cha kumeza hata nyota na vigogo wa chama cha Labour Jim Murphy, Douglas Alexander na Margaret Curran miongoni mwa wengine wengi.

Chama cha The Liberal Democrats kilipoteza viti 9 huku mwakilishi wa Orkney and Shetland Alistair Carmichael akisalia mbunge wa pekee wa chama hicho huko.

Kwa upande wao chama kinachoongoza cha The Conservatives, kilihifadhi viti vya Dumfrieshshire na Clydesdale and Tweeddale.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company