Ujumbe wa Jumuiya ya EAC watazamiwa kuwasili Burundi leo Jumatano


Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, rais wa Rwanda, Paul Kagame (kushoto) na rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni (kulia).
Reuters
Na RFI

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa Jumuia ya Afrika Mashariki amewataka mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi wanachama kufanya mazungumzo nchini Burundi, Jumatano kabla ya mkutano wa viongozi wa jumuia hiyo.



Hii ni mara ya kwanza kwa jumuia hiyo kutuma ujumbe wa ngazi ya mawaziri kwenda Bujumbura katika jitihada za kujaribu kumaliza mgogoro wa kisiasa katika nchi hiyo ambayo kwa miaka mingi imekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mawaziri hao wa jumuiya ya Afrika Mashariki wanafanya ziara hiyo mjini Bujumbura, wakati maandamnao ya raia yanaendelea kupamba moto wakipinga Pierre Nkurunziza kuwania muhula watatu wakisema ni kinyume na Katiba ya nchi hiyo pamoja na Mkataba wa amanai na maridhiano wa Arusha, ambao ni sheria mama nchini Burundi

Hatua hiyo imekuja wakati ambapo viongozi wamekosolewa kwa kukaa kimya huku hali nchini Burundi ikizidi kuwa mbaya zaidi.

Waziri wa mambo ya nje wa Burundi Laurent Kavakure alikuwa nchini Tanzania Jumatatu wiki hii ambako alifanya mazungumzo na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Tanzania Bernard Membe kabla ya kutolewa kwa taarifa hiyo.
Hata hivyo maandamano mjini Bujumbura yameendelea leo Jumatano kwa siku ya 9. waandamanaji wameapa kutositisha maandamano hayo mpaka Pierre Nkurunziza aachane na mpango wake wa kuwania muhula wa tatu.

Jumanne wiki hii Korti ya Katiba ilimruhusu Nkurunziza kuwania muhula watatu, siku moja kabla ya naibu mkuu wa Korti hiyo kuitoroka nchi, akibaini kwamba alifanyiwa vitisho vya kuuawa baada ya kupinga kutia saini kwenye uamzi wa Korti ya Katiba unaomruhusu Nkurunziza kuwania Muhula watatu. Sylvere Nimpagaritse alisema kuwa Pierre Nkurunziza hana haki ya kuwania muhula wa tatu kwani ni kinyume na Mktaba wa amani na maridhiano wa Arusha pamoja na Katiba ya nchi. Sylvere Nimpagaritse alisema majaji waliyokubaliana na uamzi huo walifanyiwa vitisho vya kuuawa na kukubali kutia saini zao kwenye waraka unaotoa uamzi huo.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company