Mji wa Malakal, Sudan Kusini, mji mkuu wa jimbo la Upper Nile, ambapo kunazalishwa kiwango kikubwa cha mafuta.
AFP PHOTO/SIMON MAINA
Na RFI
Waasi nchini Sudan Kusini wanataka kuondolewa kwa wafanyakazi katika makampuni yanayozalisha mafuta nchini humo.
Waasi hao wanaoongozwa na Riek Machar wanadai kuwa wanaelekea kumiliki maeneo yote yenye utajiri wa mafuta katika jimbo la Unity na Upper Nile lakini serikali inasema madai hayo si ya kweli.
James Gadet Dak, msemaji wa waasi amesema wameamua kuchukua udhibiti wa maeneo yote yanayozalisha mafuta na wanataka wafanyakazi kuondoka ili wasiathiriwe katika makabiliano na wanajeshi wa serikali ya Juba.
Wakati huo huo kiongozi wa kundi jipya la waasi nchini Sudan Kusini, Johnson Olony amesema waasi wake wameizamisha meli ya kijeshi katika mto Nile na kuwauwa wanajeshi 172.
Hata hivyo, serikali ya Juba imesema madai ya waasi hao hayana msingi wowote.
Hayo yakijiri wahubiri wawili raia wa Sudan Kusini wameshtakiwa nchini Sudan kwa tuhma za kuichunguza serikali.
Mawakili wao wamesema tuhma hizi kama zitathibitika wawili hao watahukumiwa adhaabu ya kifo.
Wahubiri hao Yat Michael na Peter Yen walikamatwa jijini Khartoum mwaka 2014 na mapema mwaka huu.
Yat Michael alikamatwa baada ya kuwaombea waumini wa Kanisa moja jijini Khartoum.
Idadi kubwa ya raia wa Sudan ni Waislamu huku asilimia ndogo wakiwa wakiristo.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago