Benki ya HSBC kupunguza matumizi yake

Benki ya HSBC kupunguza matumizi yake

Mojawepo ya benki kubwa zaidi duniani ya HSBC imetangaza taratibu ya kutekeleza zoezi la kupunguza matumizi yake.

Zoezi hilo litaiwezesha benki hiyo kuwasimamisha kazi zaidi ya wafanyikazi elfu ishirini kote duniani.

Benki hiyo aidha itauza baadhi ya rasilimali zake nchini Brazil na Uturuki, na kupunguza zaidi kiwango chake cha matumizi ya fedha kwa zaidi ya dola bilioni mia tatu.Benki ya HSBC kupunguza matumizi yake

Wengi wa wafanyikazi ambao watapoteza kazi watakuwa wale wa Uingereza, makao makuu ya sasa ya benki hiyo.

Uamuzi wa iwapo Benki hiyo itahamisha shughuli zake kutoka jijini London, utajulikana hatimaye mwaka huu.

Afisa mkuu mtendaji wa benki ya HSBC, Stuart Gulliver, anasema kuwa muda umewadia wa kutambua kuwa dunia imebadilika pakubwa, na kwamba ukuaji wa uchumi barani Asia sasa ndio unaofaa kuangaziwa.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company