Burundi: timu ya usuluhishi yaomba uchaguzi uahirishwe

Abdoulaye Bathily, mwakilishi wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Afrika ya Kati, akiwa pia msuluhishi mpya katika mgogoro wa Burundi.
UN Photo/Yubi Hoffmann
Na RFI

Nchini Burundi, timu ya kimataifa ya uluhishi imeitaka serikali ya Bujumbura kuahirisha uchaguzi wa wabunge na ule wa urais hadi Julai 31, ili kutafutia ufumbuzi mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini humo.

Serikali ya Burundi inatazamiwa kutoa uamzi wake leo Ijumaa iwapo itaahirisha au la uchaguzi huo. Uchaguzi wa wabunge na madiwani umepangwa kufanyika Jumatatu Juni 29, na ule wa urais umepangwa kufanyika Julai 15. Kampeni ya uchugzi wa wabunge na madiwani inamalizika leo Ijumaa jioni, na kampeni ya uchaguzi wa urais ilianza Alhamisi wiki hii.

Hata hivyo hali ya usalama imeendelea kuwa tete katika maeneo mengi nchini humo hususan katika mji mkuu wa Bujumbura. Watu wasiyojulikana waliendesha mashambulizi kadhaa ya gruneti mjini kati Bujumbura Alhamisi wiki hii, mashambulizi ambayo yalisababisha zaidi ya watu 8 kujeruhiwa.

Wakati huo huo, Alhamisi wiki hii, wanafunzi 200 wa Chuo kikuu cha taifa nchini Burundi waliingia katika majengo ya ubalozi wa Marekani mjini Bujumbura kuomba hifadhi, baada ya kuvamiwa na askari polisi katika eneo walipokua wakipiga kambi.

Wanafunzi hao wamekua wakipiga kambi tangu mwishoni mwa mwezi Aprili mbele ya ubalozi wa Marekani, ambapo walikua wakiomba ulinzi baada ya kufukuzwa katika mabweni yao wakati yalipoanza maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa rais Nkurunziza.

Mpaka Alhamisi wiki hii, wanafunzi 200 wa Chuo kikuu cha taifa ndio wamekua wakipiga kambi nje ya ubalozi wa Marekani mjini Bujumbura. Chuo hiki cha taifa kilifungwa na viongozi wa Burundi Aprili 30 wakati ambapo wanafunzi waliituhumiwa kuwa miongoni mwa waandamanaji wanaopinga muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza. Tangu wakati huo wanafunzi hao wamekua wakipiga kambi nje ya ubalozi wa Marekani mjini Bujumbura.

Polisi ilijaribu bila mafanikio kuwaondoa wanafunzi hao kwenye eneo hilo. Polisi ilikua imejiandaa kwa kutumia nguvu ili kuwaondoa wanafunzi hao. Wakati ambapo polisi ilijaribu kuwasogelea, wanafunzi hao walikusanyika kwenye mlango wa kuingilia na kupanda mlango huo kwa muda mcamche sana.

Juu ya paa za majengo ya ubalozi, kikosi cha majini cha Marekani kimeweka ngome zake. Nje ya ubalozi wa Marekani, askari polisi wa Burundi walivunja kambi ya muda iliyojengwa na wanafunzi hao. Polisi ilionekana ikipakia ndani ya gari, magodoro, masanduku na vitu vingine ambavyo viliachwa na wanafunzi.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company